Watendaji Redio za Jamii Nchini Wajengewe Uwezo – Usia Nkhoma
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma
Ledama akifafanua jinsi waandaaji wa vipindi wanavyoweza kutafuta habari
nzuri zenye kuelimisha kwa ajili ya redio za jamii na pia mbinu
wanazoweza kutumia ili kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii.
Akizungumza
katika warsha ya siku nne inayoshirikisha waandishi na maripota wa
redio za jamii inayofanyika Wilayani Sengerema mkoani Mwanza, Bi. Ledama
ameongeza kuwa upo umuhimu wa kuwajengea uwezo watendaji katika redio
hizo ikiwemo kuwafundisha namna ya kutumia mtandao wa Intaneti kwa ajili
ya kuboresha uandishi na utangazaji , haswa katika maeneo muhimu
yanayoigusa jamii ikiwemo Elimu, Afya na Kilimo na pia jinsi redio hizo
zinavyoweza kuandaa vipindi vitakavyoigusa jamii moja kwa moja.
Kwa jumla
warsha hiyo ya siku nne kwa waandishi wa habari wa redio za jamii
imeangalia kwa mapana mambo muhimu ya kijamii, na kuchambua mambo hayo
ni yapi ambapo imegusia masuala ya Afya na Kilimo pamoja na mambo
mengine na kuangali fursa zinazopatikana, pia changamoto zinazokabili
masuala hayo na kutathmini nini kifanyike ili kuboresha utendaji na
utoaji huduma katika sekta hizo.
Mtaalam wa
Kilimo kutoka Idara ya Kilimo wilayani Sengerema Bw. Joseph Manota
akizungumza katika warsha ya waandishi wa habari wa redio za jamii
inayofanyika mkoani Mwanza ambapo fursa zinazopatikana katika sekta ya
Kilimo na jinsi ya kuzitumia ili kufanikisha sera ya Serikali ya Kilimo
Kwanza na pia amezungumzia changamoto zilizopo katika kutimiza sera hiyo
na namna gani maafisa wa Kilimo pamoja na Serikali kwa ujumla wanaweza
wakafanya kukabiliana nazo ili kutimiza malengo ya kukuza Kilimo.
Mshauri wa redio za jamii kutoka Unesco Mama Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.
Pichani juu
na chini ni waandishi na maripota wa redio za jamii wanaohurudhuria
mafunzo hayo yanayofanyika kwenyen kituo cha Habari na Mawasiliano cha
Telecentre Wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Mmoja wa
watangazaji wa Redio Kahama FM William Bundala (Kijukuu cha Bibi K)
akitoa mrejesho wa mafunzo yaliyopita ambayo yameleta mabadiliko makubwa
kwa kituo chao kwa Mshauri wa Redio za Jamii kutoka UNESCO Mama Rose
Haji Mwalimu
Afisa
Elimu, Takwimu na Vifaa wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Pius Lwamimi
akizungumza na waandishi wa habari na maripota wa redio za jamii nchini
ambapo aligusia changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta Elimu wilayani
humo na kuwaasa kutumia redio zao katika kutoa taarifa muhimu kwa jamii
zitakazopelekea kukua kwa Sekta ya Elimu nchini. Pia amewataka wazazi
kuwa mstari wa mbele na kujitokeza kuhudhuria vikao katika shule na
kutoa maoni yao kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo mitaala ya elimu na pia
kushirikiana na redio za jamii kwa kutoa taarifa muhimu na pia
kuwahamasisha watoto wao na jamii nzima kujenga utamaduni wa kusikiliza
vipindi vya redio hizo kwa manufaa yao.
Sehemu ya washiriki wanaohudhuria mafunzo hayo.
Post a Comment