Mpiganaji Gracemo Bambaza Afariki Dunia



Mpiganaji Gracemo Bambaza (pichani) aliyekuwa mwandishi wa habari za michezo aliyekuwa akikitumia kituo cha Radio cha wapo Radio cha Kurasini jijini Dar es Salaam /Pride Fm ya Mtwara na  kituo cha ABM ya  Dodoma na kufanya Mafunzo ya Habari akiwa katika masomo yake ya Diploma katika kituo cha Channel 10 amefariki Dunia jana Agosti 14, 2013.  
Marehemu alikuwa akisumbuliwa na Saratani ya Koo mpaka mauti yanamkuta katika Hospitali ya Ocean Road. Marehemu alizaliwa Mwaka 1973 Mkoani Kagera na amesafirishwa leo Agosti 15, 2013 kwenda Karagwe mkoani kagera kwa mazishi. Marehemu ameacha Mke na mtoto Mmoja .
Kwa Taarifa zaidi wasiliana na Dada wa Marehemu 
Mary Mihigo 
0713 64 49 41 

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger