JESHI LA POLISI MKOA WA TANGA LINAWAKA WATU WAWILI




                          Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga.


 Na  Peter Mtulia.

Watu watatu wamefariki dunia ktk matukio tofauti ya ajali yaliyotokea maeneo tofauti jijini Tanga.

Ktk tukio la kwanza Jeshi la polisi mkoa wa Tanga linamsaka dereva wa gari aina ya fuso kwa kosa la kumgonga na kusababusha kifo cha mwendesha pikipiki aina ya farcon yenye namba za usajili T-196 BLT aliyetambulika kwa jina la Manento Juma mwenye umri wa miaka 20 pamoja na abiria wake Mwajuma Athumani mwenye umri wa miaka 30.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa polisi mkoani hapa Costantino Masawe amesema kuwa ajali hiyo imetokea mnamo siku ya alhamisi katika eneo la mambo leo  majira ya saa mbili usiku ambapo  gari hilo lilikuwa likitokea Muheza kuelekea Segera na kugongana uso kwa uso na pikipiki hiyo na kusababisha  vifo vya watu hao.

Ktk tukio la pili Mwendesha pikipiki aina ya toyo yenye namba za usajili T-445 CJJ aliyejulikana kwa jina la Asnali Saidi mwenye umri wa miaka 20 amefariki dunia  baada ya kugongwa na gari aina ya fuso katika barabara ya pangani  Tanga.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda Masawe amesema kuwa ajali hiyo imetokea mnamo siku ya ijumaa majira ya saa sita usiku katika   maeneo ya Tanga sisi na dereva wa gari hilo ametoroka kusikojulikana

Kamanda Masawe amesema kuwa jitahada za jeshi la polisi mkoa wa Tanga kuwasaka madereva wa magari hayo  zinaendelea ili kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger