CHEKI KIZAAZAA CHA KUSHINDWA KWA WAZIRI ''WILLIAM LUKUVI'' KUWATAJA WABUNGE WANAOJISHUHULISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA, YAWAKERA WABUNGE BUNGENI MJINI DODOMA. SOMA HAPA
WAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi amelazimika kufafanua kauli aliyoitoa juzi ya kuhusisha wabunge na dawa za kulevya, kwa kusema hakumaanisha kwamba wabunge wote ni
wafanyabiashara wa dawa hizo.
Lukuvi ambaye jana alisisitiza kuwa Serikali haiko tayari kutaja majina ya wafanyabiashara wa dawa hizo, aliliambia Bunge kwamba alimaanisha ipo orodha kubwa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali, yakiwemo magazeti, vyenye majina na kwamba Serikali haiko tayari, kwa kuwa inahesh
imu utawala wa sheria na mgawanyo wa majukumu.
Ufafanuzi huo aliutoa baada ya Mbunge wa Simanjiro , Christopher ole Sendeka (CCM) kumtaka kutaja majina ya watuhumiwa, wakiwemo wabunge, kama wapo, vinginevyo afute kauli yake, aliyoitoa bungeni juzi.
Akiomba mwongozo baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni, Sendeka alisema kauli iliyotolewa na Lukuvi juzi, kwamba akitaja majina ya wafanyabiashara ya unga, hakuna mbunge atakayepona ni ya kulidhalilisha Bunge kwa kuwa Watanzania kwa kauli hiyo, wanawachukulia wabunge kama wafanyabiashara hiyo.
“Naomba Mheshimiwa Waziri ataje majina hayo ili kuondoa mkanganyiko kwetu wabunge mbele ya Watanzania, vinginevyo kauli hiyo inaweza kuchukuliwa kwamba kila mbunge ni mfanyabiashara hii la sivyo afute kauli yake ya jana (juzi) aliyotoa hapa bungeni,” alisema Sendeka.
Lukuvi alisema, “Serikali inaheshimu mihimili mingine ikiwemo Polisi na Mahakama, hivyo si kazi ya Serikali kutaja tu majina kutoka kwenye orodha ya watuhumiwa. Na hilo ndilo nililosema hapa bungeni jana (juzi).
Sikuamanisha kwamba wabunge ni wafanyabiashara ya madawa ya kulevya bali nilisema katika orodha hiyo ndefu kutoka vyanzo mbalimbali, hata wabunge waliomo humu ndani ya Bunge hili hawawezi kupona kutajwa,” alisisitiza.
Kauli hiyo ya juzi ilitokana na swali la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Catherine Magige aliyetaka kufahamu sababu za biashara ya dawa hizo kukithiri nchini, huku vijana wengine wa Kitanzania wakiendelea kukamatwa kwenye viwanja vya ndege ndani na nje ya nchi.
Chanzo; gazeti la habari leo
Post a Comment