AJALI NYINGINE YATOKEA JIJINI MBEYA LEO, 10 WADAIWA KUPOTEZA MAISHA
Pichani ni Baadhi ya wakazi wa maeneo ya jirani na ilipotokea ajali hiyo wakiiangalia basi hiyo ikiwa kando kando ya mto Kiwira.
Wananchi wa Mji wa Kiwira wakienda kuangalia ajali hiyo.
Sehemu ya wananchi wa Mji wa Kiwira wakiangalia Baadhi ya Miili ya Watu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.
Taarifa
iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde toka Wilayani Rungwe, Jijini
Mbeya inaeleza kuwa Basi dogo aina ya Toyota Hiace imetumbukuia kwenye
Mto Kiwira mapema leo na inadaiwa kuwa zaid ya watu 10 waliokuwepo
kwenye basi hilo wamepoteza Maisha.
Kwa
mujibu wa mtoa taarifa, amesema kwamba ajali hii imetokea wakati Mabasi
yafanyayo safari zake kati ya Mbeya na Kyela (maarufu kama Coaster)
kugoma kutoa huduma ya kusafirisha abiria katika maeneo hayo, hivyo
baadhi ya hiace za mjini kuamua kubeba abiria, hali iliyopelekea hiace
hizo kubeba abiria wengi zaidi ya uwezo wake.
Inaelezwa
kuwa gari hiyo ilipoteza muelekea na kuingia mtoni, baada ya dereva
wake kushindwa maarifa kutokana na mwendo aliokuwa nao.
Mungu aziweke pema roho za marehemu hao,Amin.(Muro)
Post a Comment