Wakali wawili; Kaze Gilbert kulia akipata chakula cha mchana na Tambwe Amisi, Mlimani City, Dar es Salaam leo.
Na
wachezaji hao waliochelewa kwa sababu ambazo hazikuwekwa bayana,
wataungana na kikosi cha Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’
tayari kuanza kazi Msimbazi. Wawili
hao ndio pekee waliokuwa wanasubiriwa kukamilisha kikosi kizima cha
Wekundu wa Msimbazi, tayari kwa mbio za ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu. Wote
wamesajiliwa kutoka Vital’O ya Burundi, mabingwa wapya wa Klabu Bingwa
Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame katika michuano iliyofanyika
Sudan mwaka huu. Tambwe
aliibuka mfungaji bora wa mashindano hayo ambayo timu za Tanzania,
Simba SC na waliokuwa mabingwa watetezi, Yanga SC zilijitoa kwa kuhofia
machafuko yaliyokuwa yakiendelea nchini humo. Kaze
aliibuka beki bora wa mashindano hayo, yaliyoshuhudia Vital’O ikitwaa
taji lake la kwanza kabisa la michuano hiyo, licha ya kwamba ni timu
kongwe kwenye mashindano hayo ya CECAFA. Wawili
hao wanafikisha idadi ya wachezaji wanne wa kigeni wa Simba SC, kasoro
mmoja kufika kikomo kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu, baada ya Waganda,
kipa Abbel Dhaira na beki Joseph Owino. Simba
SC imepanga kukamilisha idadi ya wachezaji wa kigeni kwa kumsaini Moses
Oloya anayecheza Vietnam kwa sasa ambaye pia anawaniwa na mahasimu wao,
Yanga SC.
Post a Comment