Muheza. Wakulima wa Vijiji vya Kwemhosi, Bembe na Mtombuzi, wilayani Muheza mkoani Tanga wameiomba Serikali kuwawekea soko la uhakika la kuuzia mazao yao.
Wakizungumza mjini hapa juzi, wakulima hao walisema wamechoshwa kulanguliwa na watu waliodai ni madalali, baada ya kuwawekea vitisho vya kuacha kupeleka mazao yao masoko ya mjini.
P.T
Walitaja vitisho hivyo kuwa ni ushuru wa forodha, mapato na kutokuwa na leseni ya kufanya biashara, hivyo kulazimika kuwauzia kwa bei ya chini.
"Unajua wakulima wa vijijini tuna woga hasa unapoambiwa kuna watu wa mapato na wakamataji wasiokuwa na leseni... Hawa madalali wamekuwa wakitumia mbinu hii kujitajirisha," alisema Rukia Karata.
Na Salim Mohammed(mwananchi)
Post a Comment