skip to main |
skip to sidebar
NEWS ALART: AJALI YAUA WANNE PAPO HAPO RUFIJI
(PICHA KUTOKA MAKTABA)
WATU wanne wafanyabiashara wa nguo za mitumba wamekufa papo hapo na
wengine nane wapo mahututi baada ya gari walilokuuwa wakisafiria kutoka
mikoa ya kusini kwenda jijini Dar esalaam kuacha njia na kupinduka na
kusababisha maafa hayo.
Tukio hilo limetokea Novemba 22 asubuhi katika kijiji cha Londondo
Chumbi Tarafa ya Mohoro katika barabara kuu ya Kilwa Dar esalaam
wilayani Rufiji Mkoani Pwani
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama wa wilaya ya Rufiji Nuhudin
Babu amethibitisha tukio hilo ambapo amewataja waliokufa ni Fadhili
Chaula(55),Ally Mohamed (25),Ally Mnutu (41)pamoja na Selemani
Liangavi(45) wote wakazi wa Dar salaam.
Babu ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Rufiji amesema katika ajali hiyo
watu zaidi ya 10 walijeruhiwa lakini nane kati yao ndiyo hali zao
zilikuwa mbaya na hivyo walichukuliwa na kukimbizwa katika hospitali ya
Muhimbili Dar salaam kwa ajili ya matibabu zaidi.
Mwenyekiti huyo wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo ameeleza
kuwa ajali hiyo imehusisha gari T 198 ARQ Isuzu Forwad iliyokuwa
ikiendeshwa na Ally Mkango kutokea Newala kwenda jijini Dar esalam.
Amesema hata hivyo dereva huyo alikimbia mara baada ya kutokea tukio
hilo na kwa sasa anaendelea kutafutwa na jeshi la Polisi mkoani humo ili
kujibu tuhuma zinazomkabili.
Ameongeza kuwa msaidizi wa dereva huyo Haji Khatibu (28) anashikiliwa na
Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo na
chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kutozingatia sheria zilizopo
barabaran
Copyright © 2011.
TANGA LEO - All Rights Reserved
Post a Comment