MNENGUAJI MAARUFU 'NYAMWELA JR' ATIWA MBARONI KWA KASHFA ZA KUMLAWITI MTOTO WA KIUME WA MIAKA 6
MNENGUAJI wa kiume wa Mashujaa Band, Juma Nyamwela (Nyamwela Jr) amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa kiume wa umri wa miaka sita.Kwa sasa mnenguaji huyo yupo kituo cha polisi cha Mabatini Kijitonyama jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku ya tatu tangu akamatwe kwa tuhuma hizo.
Habari za uhakika kutoka kituoni hapo zinasema katika maelezo ya awali, mnenguaji huyo amekiri kosa.
Chanzo cha Chetu kimeeleza kuwa huenda mnenguaji huyo akafikishwa mahakamani siku ya Jumatatu.
Nyamwela ambaye ni mdogo wake na Super Nyamwela wa Extra Bongo, aliwahi kuitumikia TOT Plus kabla ya kujiunga na Mashujaa Band. Mwaka 2007 aliibuka bingwa wa mashindano ya dansa bora wa kiume yaliyoandaliwa na Usher Family na kujinyakulia zawadi ya gari.
Post a Comment