Mh Freeman Mbowe Atolewa Nje ya Ukumbi wa Bunge

Mh Freeman Mbowe Atolewa Nje ya Ukumbi wa Bunge

UKUMBI wa Bunge leo uligeuka kuwa ulingo wa ngumi baada ya wabunge wa kambi ya upinzani kutunishiana misuri na askari wa bunge hilo ambapo  Kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe alipoamliwa kutoka nje na Naibu Spika Job Ndugai.

Hatua hiyo ilitokana  baada ya wabunge hao kupiga kura za kukubali au kukataa kuhusu kupitishwa kwa kujadili Mswaada wa Katiba uliopelekwa Bungeni hapo na Serikali ili kuweza kujadiliwa na bunge hilo.

Wabunge hao wa kambi ya upinzani wakiongozwa na Freeman Mbowe walipinga matokeo hayo na kuamua kusimama na wakati huo huo Spika Ndugai aliwataka kukaa chini ili kuendelea na kuchangia hoja za msingi za kujadili mswaada huo.

Ndugai aliwataka wabunge hao kukubaliana na matokeo yaliyotokea na kwa pamoja waweze kujadili mswaada huo 
ambao ni faida kwa taifa lakini mbali na ombi hilo kambi ya upinzani walikaidi ndipo Spika alitoa dakika tano kwa za kiongozi huyo kutoka ili bunge liendelee,ambapo hata hivyo kiongozi huyo alikaidi amri hiyo.

Baada ya mabishano hayo ndipo Spika alipotumia kiti chake na kuwataka askari wamtoe kwa nguvu nje ya ukumbi wa bunge, amri ambayo ilizua taflani na hekeheka kupelekea wabunge wa kambi ya wapinzani kuungana na kuwatunishia misuri askari hao wakimkingia kiongozi huyo kutolewa nje.

Tukio hilo lililochukua dakika zaidi ya 30 lilipelekea Bw. Job Ndugai kuwatolea macho askari hao akiwaamuru kutumia mabavu ili kuweza kumtoa nje ya ukumbi Bw. Mbowe.

Sakata hilo lilifanikiwa baada ya askari hao kutii amri ya Naibu Spika huo kwa kutumia mabavu kumtoa nje kiongozi wa kambi ya upinzani ambapo aliungwa mkono na wabunge  kutoka nje ya ukumbi na kususia kikao hicho.

Katika tukio hilo Mwenyekiti wa vyama vyenye wabunge wengi bungeni na Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mkoani Kilimanjari Agustino Mrema alisema kuwa kitendo kilichofanywa na wabunge wezake si cha kungwa na na kinaleta fedheha kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Alisema yeye kutokutoka kwake nje haimaanishi kuwa ni kibaraka wa CCM na  si ndicho alichotumwa kufanya na wananchi wake,hivyo haungi mkono hata kidogo na haeleweke hivyo kuhusu msimamo wake.

"Hatoki mtu hapa nitakaa ndani ya bunge mpaka kieleweke na mnielewe kwamba mimi ndiye kiongozi wao vyama vyote tisa,hivyo nastahili kuheshimiwa na sikubaki humu ndani kwa sababu mimi ni kibaraka wa CCM bali  kinachopiganiwa ni maslahi ya taifa na ndicho nilichotumwa na wananchi wangu sikutumwa nije kutoka nje au kususia bunge."alisema Mrema.

Naye, Mbunge wa Same Mashariki na Bi Anne Kilango Malecella aliitaka Serikali kusimama imara na isiogope vitisho vinavyotolewa na wasioitakiwa mema nchi katika kupigania maslahi ya taifa.

Alisema kuwa kitendo kilichofanywa na wapinzani bungeni hakina nia njema katika kupata katiba mpya na wajumbe 156 waliopiga kura wanavigenzo vya kuweza kuchangia Mswaada huo kujadiliwa.

Vurugu za bunge hilo ziliaza toka awali katika kipindi cha muongozo wa Spika ambapo vijembe,kashifa kwa wabunge kuzungumza bila kufuata utaratibu ilimradhimu Naibu Spika Job Ndugai kusimama mara kwa mara kujaribu kurejesha utulivu katika matukio yaliyotawala Ukumbini humo. 





Mara baada ya kutolewa mwongozo ulioombwa na wabunge juzi wakidai Muswada wa Mabadiliko ya rasimu ya katiba umeingizwa vipengele kinyemele, na Zanzibar kutoshirikishwa kikamilifu, wabunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni na wale wa CCM walikuwa wakituhumiana kusema uongo kuhusiana na hatua hiyo ya uandaaji wa mchakato wa Rasimu wa Katiba mpya.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger