Mji mkuu wa Misri Cairo ulitumbukia katika ghasia Ijumaa(16.08.2013)
wakati watu waliokuwa wakilinda doria katika vizuwizi vilivyowekwa
katika vitongoji vya mji huo walipopambana na waandamanaji.
Mapigano makali kabisa ya mitaani ambayo hayajawahi kuonekana mjini Cairo katika muda wa zaidi ya miaka miwili ya ghasia yamesababisha kiasi watu 82 kuuawa, ikiwa ni pamoja na maafisa wa polisi.
Mapambano ya silaha.
Wakaazi wamekuwa wakifyatuliana risasi na kuashiria mwelekeo mbaya katika mzozo huo, wakati raia ambao walikuwa na bastola na bunduki walipopambana na waandamanaji waliokuwa wakishiriki kile ambacho kundi la Udugu wa Kiislamu ilikiita "siku ya hasira" , iliyozushwa na hasira dhidi ya majeshi ya usalama kuwaondoa kwa nguvu waandamanaji waliokuwa wamekita kambi katika maeneo mawili mjini Cairo siku ya Jumatano na kuzusha mapambano ya nchi nzima ambapo watu zaidi ya 600 walipoteza maisha.
Kundi la Udugu wa Kiislamu linaendeleza upinzani dhidi ya jeshi
Maandamano zaidi
Udugu wa Kiislamu wakionyesha ukaidi wameitisha wiki ya maandamano nchini Misri kuanzia leo Jumamosi.Majeshi ya usalama na raia kadhaa waliuzingira msikiti wa al-Fateh katikati ya jiji la Cairo katika eneo la Ramses ambako waandamanaji wa kundi la Udugu wa Kiislamu walikimbilia kujisalimisha wakati wa mapambano hayo siku moja kabla.
Waandamanaji wakifyatuliwa mabomu ya kutoa machozi
Idadi ya waliokamatwa ikiwa ni wafuasi wa kundi la Udugu wa Kiislamu imefikia 1004, taarifa hiyo imesema , mjini Cairo pekee wakiwa wamekamatwa watu 558. Mapambano hayo yamesababisha zaidi ya watu 80 kupoteza maisha, kwa mujibu wa maafisa na watu waliokuwa wakishuhudia katika eneo lililowekwa la muda la kuhifadhi maiti.
Umoja wa Ulaya kujadili ghasia Misri
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamezungumza jana Ijumaa (16.08.2013) juu ya haja ya jibu la pamoja la ghasia nchini Misri na kukubaliana kuitisha mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja huo wiki ijayo.
Maiti zikiwa zimepangwa msikitini
Taarifa ya serikali ya Ujerumani imesema kuwa Merkel amemwambia rais wa Ufaransa Hollande kuwa Ujerumani, moja kati ya mshirika mkubwa wa kibiashara na Misri , itaangalia upya uhusiano wake na Misri kuhusiana na umwagaji damu uliotokea wiki hii.
Post a Comment