IVORY COAST NAYO YAFUZU KOMBE LA DUNIA BAADA YA SARE YA1-1 NA SENEGAL
YAUNGANA NA NIGERIA KUWA TIMU MBILI ZA KWANZA KUFUZU FAINALI HIZO KUTOKA AFRIKA
TIMU ya taifa ya Ivory Coast imefuzu Fainali zijazo za Kombe la Dunia baada ya sare ya 1-1 usiku huu ugenini na Senegal kwenye Uwanja wa Mohamed V in Casablanca, Morocco.
Matokeo hayo yanaifanya Didier Drogba na wenzake wafuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-2 na kuungana na Nigeria iliyoitoa kwa jumla ya mabao 4-1 Ethiopia.Ikiwa inajivunia ushindi wa 3-1 katika mchezo wa kwanza, Tembo walilazimika kusota kusawazisha bao baada ya Moussa Sow kutangulia kuwafungia Simba wa Teranga kwa penalti, kabla ya Salomon Kalou kusawazisha dakika za majeruhi.
Kikosi cha Senegal: Coundoul, S. Sane, L. Sane, Mane, Badji/Saivet dk82, P. Cisse, Mbodji, Gueye, Souare, Djilobodji na Ndoye/Sow 66.
Ivory Coast: Barry, K. Toure, Bamba, Gosso, Zokora, Romaric, Aurier, Y. Toure, Kalou, Gervinho/Sio dk80 na Drogba
Post a Comment