Butiku anena; ningejua CCM itaingilia mchakato wa Katiba nisingeshiriki
Mjumbe wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Joseph Butiku amesema asingekubali
kushiriki katika Tume hiyo laiti kama angejua CCM ingeingilia mchakato
huo.
Butiku
ambaye alitoa kauli hizo kwa nyakati tofauti, wikiendi iliyopita kwenye
Mabaraza ya Katiba ya Halmashauri ya Mji wa Soni, Lushoto na Halmashauri
ya Wilaya ya Handeni, alieleza kutokufurahishwa kwake na kitendo cha
CCM kushinikiza maoni yake mbele ya mabaraza hayo.
Alilalamika
kuwa kitabu cha mwongozo wa utoaji maoni kilichotolewa na CCM
kinatumiwa vibaya kushinikiza maoni kwenye Rasimu ya Katiba Mpya.
"CCM
imeandaa kitabu kizuri kweli kusaidia wanachama wake, tuliwaambia (Tume)
hatukitaki; ni mwongozo kusaidia wanachama wake namna ya kutoa maoni,
lakini kimekuwa kinatumika vibaya. Kinatumika kushinikiza maoni,"
alisema Butiku.
Butiku
ambaye ni mwanachama wa Tanu tangu mwaka 1958 na CCM kuanzia 1977
alisema: "Ningejua itatokea chama kitafanya hivyo, nisingekula kiapo
nilichokula kufanya kazi hii katika Tume ya Marekebisho ya Katiba. Kundi
moja lisigeuke Tanzania.
Mimi ni mzee nasema kitu kikubwa nataka
Mwenyekiti (wa CCM) asikie, Halmashauri Kuu yangu (ya CCM) isikie.
Mchakato huu usiingiliwe, madiwani saidieni wananchi wenu kujielewa.
Muungano hautaponywa kwa helikopta zinazoruka au vitabu
vinavyosambazwa."
Muungano.
Kuhusu
Muungano, Butiku aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini
alisema: "Mimi ni mzee sasa, sitaki kwenda kaburini bila kuwaambia
ukweli. Endeleeni kuujadili, msifanye jambo la kutaka asali bila kujua
madhara yake," alisema.
Kauli
hiyo ya Butiku ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mfuko wa Mwalimu
Nyerere ilitokana na wajumbe kuonyesha mvutano kuhusu muundo wa Serikali
katika Muungano na wengi walionekana kuelemea upande wa Serikali mbili
uliopo sasa, baadhi kuunga mkono Rasimu ya Katiba inayopendekeza
Serikali tatu, huku wachache wakitaka Serikali moja.
Butiku
aliwataka wajumbe wa Mabaraza ya Katiba kutoa maoni yanayolenga kulinda
na siyo kuvunja Muungano na kwamba Tume ya Marekebisho ya Katiba imepewa
kazi ya kuulinda akisisitiza kwamba haikuwa, wala haina ajenda ya
kuvunja.
"Wapo pia
viongozi wakubwa ndani ya Baraza la Wawakilishi, wengine wamestaafu,
hawautaki Muungano. Tume inawafahamu wanaotaka Tume ya Katiba iwe na
ajenda ya kuvunja Muungano. Muungano huu, ulimfukuza Aboud Jumbe
madarakani, kiongozi mkubwa tu, mi nawaambia mambo mengine siri. Jumbe
alitoka kwenye mkutano wa CCM, kaja pale nje akakuta gari lake lingine
siyo la Makamu. Leo, (anamtaja kiongozi huyo) anasema tulifanya makosa
kuungana, anajiunga na Jumbe, anaanza kufanana na Uamsho," alisema
Butiku.
Butiku
aliifananisha Katiba Mpya nzuri kuwa sawa na asali akieleza kuwa
inahitaji umakini wakati wa kuiandaa, akifafanua kuwa unapoandaa asali
lazima uwe makini vinginevyo unaweza kuambulia kushambuliwa na nyuki.
"Wajumbe
msipokuwa wa kweli, badala yake watu wakaumwa na nyuki, mtatulaumu.
Ukweli wanaufahamu wote ili waweze kuamua? Tumekubaliana kwenye Tume
tuambiane ukweli ili tupate asali:CHANZO MWANANCHI.
Post a Comment