Hii ya binti wa miaka 14 kujifungua Mapacha watatu Kenya umeisoma yote?


Hii ya binti wa miaka 14 kujifungua Mapacha watatu Kenya umeisoma yote?

Kenya 

Radio station ya Kenya ‘Radio Maisha’ imeripoti kwamba wauguzi katika hospitali kuu ya Bungoma nchini humo wamepigwa na butwaa baada ya msichana mwenye umri wa miaka 14 kujifungua mapacha watatu.

Madaktari katika hospitali hiyo wanasema kuwa watoto hao wako katika hali nzuri ya afya japo mama yao bado anaonekana kuwa mnyonge.

Afisa wa baraza la kaunti ya Bungoma anayesimamia afya Grace Khayota, aliwaongoza maafisa wengine wa kaunti hadi hospitali hiyo kuwaona watoto hao ambapo sasa mama wa watoto hao Mwanarahab Wamukoya ambae ni msichana wa miaka 14, ameomba Wasamaria kumpa usaidizi kwenye kuwalea watoto.

Taarifa kwenye sentensi nyingine imesema binti huyu wa miaka 14 amepata watoto hao kutokana na uhusiano wa kimapenzi kati yake na mpenzi wake ambae ni mvulana wa miaka 16.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger